MICHEZO NA BURUDANI
Timu ya Real Madrid imerudi kileleni usiku wa jana baada ya timu ya Barcelona kuongoza kwa mda. Timu hiyo imerudi kileleni
baada ya kuichapa Villareal 3-2. Madrid ilifanya hivyo iktokea nyuma kwa magoli mawili kwa sifuri.Villareal walifunga magoli yao mnamo dakika ya 50 na 56 kupitia Trigueros Muñoz na Bakambu lakini Gareth Bale akaipa Bao Real Dakika ya 64.
Kisha Real wakapata Penati baada ya Mchezaji wa Villareal Bruno kuunawa Mpira na Cristiano Ronaldo kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 74. Bao la 3 na la ushindi kwa Real lilipachikwa Dakika ya 83 na Alvaro Morata alienzia Benchi Mechi hii.
Matokeo hayo yamewapa uongozi Real wakiwa na Pointi 55 kwa Mechi 23 na Barca ni wa Pili wakiwa na Pointi 54 kwa Mechi 24.
Timu ya 3 ni Sevilla wenye Pointi 52 kwa Mechi 24
Golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye kwa sasa anaichezea timu ya Kagera Sugar ya Bukoba Juma Kaseja ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi January wa Ligi Kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.
Kaseja ametangazwa mshindi wa tuzo hiyo aliyokuwa anawania na wachezaji wengine wawili, ambao ni Mbaraka Abeid anayecheza nae Kagera Sugar na Jamal Mtengeta anayeichezea Toto African ya Mwanza, Kaseja sasa atapewa zawadi ya Tsh milioni moja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo yaai kampuni ya vodacom.
Takwimu zinaonexha kua golikipa huyo timu ya simba na baadae yanga na kwa sasa ni kipa wa kagera sugar kafungwa goli moja katika mechi zao tatu za January, huku timu yake ikifunga magoli 6.
Comments
Post a Comment