Kivumbi leo kinatimka tena kwenye uwanja wa Estádio do Dragão pale Porto mjini. Kocha Massimiliano Allegri wa Juventus imekipanga kikosi cha akina Buffon; Lichtsteiner, Rugani, Chiellini, Alex Sandro; Pjanić, Khedira; Cuadrado, Dybala, Mandžukić; Higuaín kuanza uwanjani wakati atayekuwa nje bila kucheza ni Bonucci kwa utovu wa nidhamu. Wakati huo huo, kocha Nuno Espírito Santo wa FC Porto anatarajia kuwaanzisha akina Casillas; Maxi Pereira, Marcano, Felipe, Alex Telles; Danilo, Herrera, Óliver Torres; Brahimi, André Silva, Soares na wala hakuna ambaye hatocheza.
Comments
Post a Comment