REAL MADRID WALAZIMISHWA SARE
Timu ya Real Madrid imeshindwa kutamba jana kwenye uwanja wao wa nyumbani mara baada ya kulazimisha sare ya bao 3-3 dhidi ya Las Palmas. Real Madrid walikua wa kwanza kupata goli lao mnamo dakika ya 8 kupitia kwa mchezaji wao Isco hata hivyo goli hilo halikudumu kwani mnamo dakika mbili baadae Las Palmas walichomoa goli hilo kupitia kwa Tana aliefunga dakika ya 10. Mchezo uliendelea vizur mpaka kufikia dakika ya 47 ambapo Real Madrid walipata pigo mara baada ya mchezaji wao tegemezi Gareth Bale kutolewa kwa kadi nyekundu. Na mara baada ya hapo Madrid walionekana kuelemewa na kupelekea Las Palmas kupata goli dakika ya 56 kupitia mchezaji wao J.Viera na dakika ya 59 walipta goli la tatu kupitia mchezaji wao Boateng. Hata hivyo Madrid hawakukata tamaa na hatimae mnamo dakika 86 na 89 Real Madrid walipata magoli mawili kupitia mchezaji wao C. Ronaldo na kufanya matokeo kua 3-3. kwa matokeo hayo basi yanawafanya Real Madrid kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi yao wakiwa nyuma kwa point mbili dhidi ya vinara wa ligi hiyo kwa sasa FC BARCELONA lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Comments
Post a Comment