LEICESTER CITY YANG'ARA NYUMBANI

Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama EPL wameibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 3-1 dhidi ya timu ya jiji la Hull. Hull city walikua wa kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji wao S.Clucas mnamo dakika ya 14 na baadae mabingwa hao watetezi wa EPL walirudisha goli mnamo dakika ya 28 kupitia mchezaji wao C.Fuchs matokeo yakabaki hivyo mpaka kipindi cha kwanza kuisha. Mara baada ya kurudi kipindi cha pili mchezaji tegemezi kabisa Riyad Mahrez aliiandikia Leicester city goli la pili mnamo dakika ya 59 na baadae dakika chache kabla ya mpira kuisha dakika ya 90 walipata goli la tatu kupitia mchezaji T. Huddlestone na kufanya mchezo kuisha kwa Leicester kushinda goli 3-1

Matokeo mengine ni kua stoke city 2- middlesbrough 0, West Brom 0-2 crystal palace, Swansea 3-2 Burnley, Watford 3-4 Southampton.

Comments

mhinda blog

Popular posts from this blog

VIKOSI VITAKAVYOCHEZA FC PORTO VS JUVENTUS HIVI HAPA