REAL MADRID WARUDI KILELENI

Timu ya Real Madrid imerudi kileleni usiku wa jana baada ya timu ya Barcelona kuongoza kwa mda. Timu hiyo imerudi kileleni
baada ya kuichapa Villareal 3-2. Madrid ilifanya hivyo iktokea nyuma kwa magoli mawili kwa sifuri.

Villareal walifunga magoli yao mnamo dakika ya 50 na 56 kupitia Trigueros Muñoz na Bakambu lakini Gareth Bale akaipa Bao Real Dakika ya 64.
Kisha Real wakapata Penati baada ya Mchezaji wa Villareal Bruno kuunawa Mpira na Cristiano Ronaldo kufunga Penati hiyo katika Dakika ya 74. Bao la 3 na la ushindi kwa Real lilipachikwa Dakika ya 83 na Alvaro Morata alienzia Benchi Mechi hii.
Matokeo hayo yamewapa uongozi Real wakiwa na Pointi 55 kwa Mechi 23 na Barca ni wa Pili wakiwa na Pointi 54 kwa Mechi 24.
Timu ya 3 ni Sevilla wenye Pointi 52 kwa Mechi 24

Comments

mhinda blog

Popular posts from this blog

VIKOSI VITAKAVYOCHEZA FC PORTO VS JUVENTUS HIVI HAPA