MBUNGE WA BABATI ANUSURIKA KIFO
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo
baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na
kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu
waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge
wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa
katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa
kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira
amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani
ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati
kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya
kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni
200.
Comments
Post a Comment