MAN U BINGWA EFL
Klabu ya Menchester United imetwaa Kombe la EFL mwaka 2017. Man U imetwaa
kombe hilo kwa kuwafunga Southampton magoli 3 kwa 2. Magoli ya Manchester yamefungwa na Zlatan Ibrahimovich dakika ya 19 na 87. Goli la pili lilifungwa dakika ya 38 na Lingard.
Kwa upande wa Southampton, magoli yote mawili yalikuwa na kusawazisha. Dakika ya 45 na dakika ya 48 baada ya muda mchache tu kutoka mapumziko, Gabbiadini alipachika mabao hayo.
Mchezo ulikuwa mgumu hasa baada ya kutoka mapumziko ambapo Southampton walioonekana kumiliki mpira kwa muda mrefu kuliko Man U. Lakini mpaka mpira unakaribia kuisha Ibra akawanyanyua mashabiki wa Mashtani wekundu kwa kugonga kichwa matata na kuifanya Man U kutwaa ubingwa huo.
Comments
Post a Comment